Exodus 30:22-32

Mafuta Ya Upako

22 aKisha Bwana akamwambia Mose, 23 b“Chukua vikolezi bora vifuatavyo: shekeli 500
Shekeli 500 ni sawa na kilo 6.
za manemane ya maji, shekeli 250
Shekeli 250 ni sawa na kilo 3.
za mdalasini wenye harufu nzuri, shekeli 250 za miwa yenye harufu nzuri,
24 eshekeli 500 za aina nyingine ya mdalasini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, pia hini
Hini moja ni sawa na lita 4.
ya mafuta ya zeituni.
25 gVitengeneze vikolezi hivi kuwa mafuta matakatifu ya upako yenye harufu nzuri, kazi ya mtengeneza manukato. Yatakuwa mafuta matakatifu ya upako. 26 hKisha yatumie kupaka hilo Hema la Kukutania, Sanduku la Ushuhuda, 27meza na vifaa vyake vyote, kinara cha taa na vifaa vyake vyote, madhabahu ya kufukizia uvumba, 28madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na vyombo vyake vyote na sinia pamoja na kitako chake. 29 iUtaviweka wakfu ili viwe vitakatifu sana na kila kitakachoigusa kitakuwa kitakatifu.

30 j“Mtie Aroni na wanawe mafuta na uwaweke wakfu ili waweze kunitumikia katika kazi ya ukuhani. 31 kWaambie Waisraeli, ‘Haya yatakuwa mafuta matakatifu yangu ya upako kwa vizazi vijavyo. 32Usiyamimine juu ya miili ya wanadamu wala usitengeneze mafuta ya aina nyingine kwa utaratibu huu. Ni mafuta matakatifu na ni lazima myaone kuwa ni matakatifu.
Copyright information for SwhNEN